IQNA

Filamu kuhusu "Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu" yaonyeshwa na Al Jazeera

11:50 - December 21, 2008
Habari ID: 1720970
Filamu kuhusu "Jumba la Makumbusho ya Sanaa za Kiislamu" iliyotengenezwa na Akram Udwani imeonyeshwa na kanali ya televisheni ya Al Jazeera.
Filamu hiyo inayolenga kuarifisha majumba ya makumbusho ya sanaa za Kiislamu nchini Qatar ilionyeshwa mara tatu katika sherehe za ufunguzi wa "Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu" na inatazamiwa kuonyeshwa tena katika kanali hiyo wiki ijayo.
Filamu hiyo inaonyesha nukta mbalimbali kuhusu jumba hilo la makumbusho kama vile usanifu majengo wake unaovutia hasa kuba lake.
Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu lililoko huko Doha, Qatar lina athari za sanaa na ustaarabu wa Kiislamu kuanzia miaka 1400 iliyopita. Athari hizo zimekusanywa kutoka maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu. 335835





captcha