IQNA

Makundi yenye misimamo mikali yameuchoma moto msikiti wa Lyon

10:50 - December 23, 2008
Habari ID: 1721860
Moto uliotokea katika msikiti wa eneo la Saint-Priest katika viunga vya mji wa Lyon nchini Ufaransa na hujuma dhidi ya makaburi ya Waislamu huko kaskazini mwa nchi hiyo ni vitendo vinavyotekelezwa kwa mpangilio maalumu na mkundi ya kisiasa yenye fikra za kibaguzi na misimamo mikali.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kidini wa Aljeria Bu Abdullah Ghulamullah ambaye ameongeza kuwa, si sahihi kwamba viongozi wa serikali ya Ufaransa ndio waliowasha moto katika msikiti huo.
Ghulamullah mesema: Makundi ya kisiasa yenye misimamo mikali na fikra za kibaguzi yanapinga suala la kuwepo uhusiano mzuri na maisha ya amani kati ya wafuasi wa dini na tamaduni tofauti na hayaheshimu haki za binadamu na za kiraia. Waziri wa Waqfu wa Aljeria amesisitiza kuwa, vitendo viovu vya makundi ya kibaguzi na yenye misimamo mikali ya Ufaransa dhidi ya vituo na taasisi za Kiislamu vinakwamisha mwenendo wa kuimarisha uhusiano mzuri na maisha ya amani kati ya wafuasi wa dini mbalimbali nchini Ufaransa. 337011
captcha