IQNA

Uislamu ndiyo sababu ya kuchanua kiuchumi mji wa Guangzhu, China

12:41 - December 25, 2008
Habari ID: 1722640
Wafanyabiashara wa Kiislamu wametajwa kuwa ndiyo sababu ya kuchanua kiuchumi mji wa Guangzhu nchini China.
Mji huo ambao unatambuliwa kuwa kituo cha kimataifa cha biashara huko kusini mwa China na wenye idadi kubwa ya Waislamu, umekuwa ukitembelewa na idadi kubwa ya wafanyabiashara wa Kiislamu kutoka Mashariki ya Kati, Afrika, Asia kusini na kaskazini katika miaka ya hivi karibuni, suala ambalo limestawisha zaidi uchumi wa eneo hilo.
Uislamu uliingizwa kwa mara ya kwanza katika mji wa Guangzhu na wafanyabiashara karibu miaka elfu moja iliyopita na kwa mujibu wa ripoti ya Jumuiya ya Kiislamu ya mji huo, Waislamu kati ya elfu 50 hadi 60 wa Kichina wanaishi katika mji huo.
Mji wa Guangzhu una misikiti minne mikubwa ambayo hutumiwa na zaidi ya Waislamu elfu 10 kwa ajili ya swala za Ijumaa. Vilevile una hoteli za vyakula vya halali katika maeneo yenye raia wengi wa Kiislamu ambayo hupika vyakula vya Kichina, Kiafrika, Kiarabu na Kithailandi. 337909

captcha