IQNA

Mazungumzo ya Iran na Waarabu ni ya dharura kwa ajili ya kutatua migogoro

16:34 - December 27, 2008
Habari ID: 1723286
Amr Musa,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa mazungumzo na mashauriano kati ya Iran na nchi za Kiarabu yana umuhimu mkubwa katika kutatua matatizo ya kieneo na kimataifa zikiwemo juhudi za kutatua mzozo na mzingiro wa Ukanda wa Gaza huko katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
Shirika Rasmi la Habari la Kuwait KUNA limemnukuu Amr Musa akisema kuwa, kutokuwepo mazungumzo ya pande mbili hizi kumepelekea kupenya na kuingia wageni katika eeo nyeti la Mashariki ya Kati na kuchochea uadui kati ya nchi hizi za Kiislamu. Amesema, kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza ni aina mbovu zaidi ya ukaliwaji wa mabavu wa ardhi za Waarabu na kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu hadi sasa imefanya juhudi kubwa za kuvunja mzingiro huo na wakati huohuo kukomesha mashambulio ya kinyama yanayotekelezwa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina katika maeneo mbalimbali ya ardhi za Wapalestina.
Amr Musa mwishoni amekemea vikali msimamo dhaifu wa baadhi ya watawala wa Kiarabu kuhusiana na mzingiro huo wa Gaza na kuzitaka nchi za Kiislamu na Kiarabu kuchukua msimamo mmoja imara katika kukabiliana na hatua za kinyama za utawala huo dhidi ya wakazi wasio na hatia wa Gaza. 338428
captcha