IQNA

Kipindi cha “Sauti ya Waislamu Mjini Washington” katika redio ya WUST

11:30 - December 28, 2008
Habari ID: 1723600
Kipindi cha kila wiki cha “Sauti ya Waislamu Mjini Washington” kinaanza kurushwa hewani leo kupitia Redio ya WUST katika mji mkuu wa Marekani, Washington.
Msimamizi wa kipindi hicho Mahdi Brai amesema kuwa, kipindi cha Sauti ya Waislamu Mjini Washington kina dakika 30 na kitakuwa kikirushwa hewani kila siku ya Jumapili. Amesema kuwa lengo la kipindi hicho ni kuonyesha sura halisi ya dini tukufu ya Kiislamu kwa wananchi wa Marekani na kutoa majibu kwa maswali na tuhuma zinazonasibishwa kwa dini hiyo na wafuasi wake.
Mahdi Brai Amesema, sehemu ya kwanza ya kipindi cha Sauti ya Waislamu Mjini Washington itamkaribisha Keith Morris Ellisson, mbunge wa kwanza Muislamu katika Congresi ya Marekani na itajadili changamoto zinazowakabili Waislamu na hali ya Waislamu waliowachache nchini Marekani.
Ameongeza kuwa kutangazwa kipindi hicho ni hatua muhimu katika njia ya kutatua matatizo ya Waislamu nchini Marekani na kwamba, kipindi hicho cha kila wiki kitajadili masuala mbalimbali ya kidini, kisiasa, kiutamaduni, uchumi wa Kiislamu na masuala ya haki za kiraia. 338791
captcha