IQNA

Jumuiya ya Kiislamu ya Uingereza yataka kusimamishwa mara moja mauaji ya kinyama katika Ukanda wa Gaza

12:59 - December 28, 2008
Habari ID: 1723719
Jumuiya ya Kiislamu nchini Uingereza imetoa taarifa ikilaani vikali mashambulio yaliyofanywa jana Jumamosi na utawala haramu wa Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza na kutaka kusimamishwa mara moja mashambulio hayo yanayofanywa dhidi ya raia wasio na hatia.
Mkuu wa jumuiya hiyo Ahmad ar-Rawi ametahadharisha katika taarifa hiyo kuhusiana na matokeo mabaya na hatari ya mashambulio hayo ya kinyama dhidi ya wananchi wa Palestina. Ameongeza kuwa, askari ghasibu wa QudsTukufu baada ya kupita mwaka mmoja wa kuzingirwa Ukanda wa Gaza jana waliamua kuwaua kwa umati wanawake, watoto, vijana na wazee wasio na hatia kwa kuyashambulioa kwa ndege za kivita maeneo mbalimbali ya Ukanda huo. Ameendelea kusema kuwa, mashambulio hayo ni mfano wa wazi wa jinai dhidi ya binadamu na ukiukaji ulio bayana wa misingi na sheria za kimataifa pamoja na thamani za kiutu. Amezitaka taasisi na mashirika yote muhimu ya kimataifa na hasa Umoja wa Mataifa kufanya juhudi za kutosha ili kusimamisha jinai hizo za utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia. Ametahadharisha juu ya uwezekano mkubwa wa kutokea janga la kibinadamu katika Ukanda wa Gaza na kuitaka serikali ya Uingereza pamoja na Umoja wa Ulaya kufanya kila liwezekanalo kwa ajili ya kulaani na kusimamisha mara moja mauaji hayo ya umati. Ar-Rawi pia amezitaka jumuiya na mashirika ya Kiislamu kutuma mara moja misaada ya kibinadamu huko Gaza kwa madhumuni ya kuwasaidia wakazi wa ukanda huo wanaoendelea kuteseka chini ya hujuma ya kijeshi na mzingiro wa Wazayuni. 339319
captcha