Shirika Rasmi la Habari la Kuwait KUNA, limesema kuwa baraza hilo la Kiislamu limesema katika taarifa hiyo iliyotolewa huko Brussels Ubelgiji kwamba, Waislamu wa Ulaya wanafuatilia kwa karibu matukio ya kusikitisha yanayotokea katika ukanda huo dhidi ya raia wasio na hatia. Taarifa hiyo imezitaka jumuiya na mashirika ya Kiislamu ya nchi mbalimbali za Ulaya kuandaa maandamano katika vituo vya Kiislamu na misikiti ili kulalamikia jinai na unyama huo unaotekelezwa na Wazayuni dhidi ya raia wasio na hatia. Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo, Baraza la Kiislamu la Ulaya limezitaka nchi za Kiislamu kuchukua msimamo mmoja katika kukabiliana na mauaji ya Israel huko Gaza na kufanya kila juhudi ili kusimamisha mashambulio hayo na kuondoa mzingiro unaotekelezwa kidhulma na Israel dhidi ya ukanda huo. Katika hali ya hivi sasa zaidi ya mashirika na jumuiya 100 za Kiislamu ni wanachama wa baraza hilo. 340021