IQNA

Seneti ya Mauritania yataka kufukuzwa nchini humo balozi wa Israel

10:14 - December 30, 2008
Habari ID: 1724775
Seneti ya Mauritania imefanya kikao cha dharura kwa ajili ya kuchunguza hali hatari ya Ukanda wa Gaza na kutaka kufukuzwa mara moja balozi wa utawala haramu wa Israel kutoka nchini humo na kuitwa nyumbani balozi wake aliyeko huko Tel Aviv.
Seneti hiyo wakati huohuo imetangaza uungaji mkono wake kwa taifa madhlumu la Palestina na kuzitaka nchi za Kiarabu kufanya kikao cha dharura kwa ajili ya kuvunja mzingiro unaotekelezwa na Israel dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza. Seneti hiyo ya Mauritania imelaani vikali msimamo wa Marekani na taasisi za kimataifa wa kupuuza mzingiro wa Gaza na mashambulio ya kinyama yanayofanywa na Wazayuni dhidi ya raia wasio na hatia katika ukanda huo. Katika upande wa pili, maelfu ya wananchi wa Mauritania wameitikia wito uliotolewa na makundi ya kisiasa na kijamii ya nchi hiyo kwa kufanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, ambapo wametaka kukatwa uhusiano wa kidiplomasia wa nchi hiyo na utawala haramu wa Israel. Mauritania ni nchi ya tatu ya Kiarabu kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel, lakini katika siku za hivi karibuni na kufuatia jinai na mauaji ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina huko Gaza, wananchi na taasisi za serikali ya nchi hiyo zimekuwa zikitaka kufukuzwa mara moja balozi wa utawala wa Israel nchini humo. 340070
captcha