Akitoa taarifa yake ya tatu kufuatia mashambulio ya anga ya utawala ghasibu wa Israel huko Gaza, Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekosoa vikali uzembe wa viongozi wa ulimwengu katika kutatua mgogoro wa Ukanda wa Gaza na hivyo kuufanya utawala huo uendelee kutekeleza mauaji yake ya kinyama dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
Amesema kuwa juhudi zinazofanywa na viongozi hao kwa ajili ya kuutatua mgogoro huo hazitoshi. Ban Ki-moon amewataka watawala wa nchi za Kiarabu na nchi za Magharibi kufanya jitihada zaidi ili kumaliza mzingiro unaotekelezwa na Israel huko Gaza na kusimamisha mara moja mashambulio yake dhidi ya wakazi wa ukanda huo. Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amezitaka nchi zote husika kutumia njia za kisiasa ili kutoa mashinikizo dhidi ya utawala wa Israel na kuufanya usimamishe mara moja mashambulio yake katika Ukanda wa Gaza. Taarifa ya katibu mkuu huyo pia imewataka Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiarabu kuchukua msiammo wa pamoja kuhusiana na mzozo wa Gaza na kuchukua maamuzi madhubuti katika kikao chao cha siku ya Jumatano huko Cairo kwa lengo la kusimamisha mashambulio ya kinyama ya Israel dhidi ya raia wasio na ulinzi wa Gaza. 340811