Kufuatia tangazo hilo, serikali ya Qatar imeandaa mipango ya hafla na tamasha za kitamaduni na kidini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Turathi ya Qatar, mji wa Doha umeandaa mipango mbalimbali mwakani. Harakati hizo za kitamaduni zitajumuisha maonyesho, vikao, makongamano na tamthilia. Mojawapo ya malengo ya tamasha hizo ni kuarifisha utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu kwa walimwengu.
Katika kujitayarisha kwa ajili ya tamahsa hizo za mwaka 2010, mwezi huu wa Januari kutafanyika kikao mjini Doha ambacho kitajadili suala la lugha ya Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu.
Itakumbukwa kuwa tarehe 24 Disemba kulifanyika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu mjini Doha ambayo yalihesabiwa kuwa mojawapo ya mikakati ya kuutayarisha mji huo kwa ajili ya tamasha za kiutamaduni za mwaka 2010.
Mji wa Quds katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu ndio uliochaguliwa kuwa mji mkuu wa kitamaduni katika ulimwengu wa Kiarabu mwaka huu wa 2009. Katika kuunga mkono mji huo, Qatar imechapisha stampu na vitabu kuhusu Quds Tukufu. Aidha moja kati ya barabara za mji wa Doha imepewa jina la Quds.
809876