Kwa mujibu wa gazeti la al Mustaqbal la Beirut, katika kikao kilichohudhuriwa na Rais Michel Suleiman wa Lebanon, mawaziri hao wamesema, kuna haja ya viongozi wa nchi za Kiarabu kukutana haraka ili waweze kuchukua msimamo wa pamoja na unaofaa kuhusu jinai zinaozedelea kufanywa na Wazayuni huko Gaza. Aidha Baraza la Mawaziri la Lebanon limeitaka jamii ya kimataifa kutekelezwa majukumu yake kuhusiana na mkasa wa Gaza.
Katika kikao chake cha Jumanne, Baraza la Mawaziri la Lebanon lililaani vikali jinai zinazotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na kuongezwa kuwa, Israel inapaswa kubebeshwa lawama zote za jinai za Gaza. Baraza la Mawaziri la Lebanon pia limeidhinisha bajeti ya dharura ya dola milioni moja za Kimarekani kwa ajili ya kuwasaidia wakazi wa Ukanda wa Gaza ambao nyumba zao zimebomolewa kwa mabomu ya Wazayuni. Wananchi wa Lebanon aidha wametakiwa kutoa mchango wao wa kifedha kwa ajili ya kuwasaidia raia wanaodhulumiwa wa Gaza. 341693