IQNA

Baraza la Usalama linapasa kuuarifisha utawala wa Israel kuwa wa kivamizi

11:08 - January 03, 2009
Habari ID: 1726384
Mabalozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu walioko huko Geneva Uswisi wametoa taarifa wakilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuuarifisha utawala haramu wa Israel kuwa utawala vamizi na unaozikalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina.
Katika taarifa hiyo, mabalazi hao wamesisitiza kwamba mashambulio ya kinyama yanayofanywa na utawala ghasibu wa Isreal huko katika Ukanda wa Gaza dhidi ya raia wasio na hatia wala ulinzi ni ukiukaji wa wazi wa sheria na maazimio ya kimataifa na hasa azimio la Geneva. Taarifa hiyo imeutaka utawala huo haramu kuheshimu sheria za kimataifa kuhusiana na haki za binadamu, kulindwa kwa maisha ya raia, kuondoa mara moja mzingiro unaoutekelezwa dhidi ya Ukanda wa Gaza na kukomesha mauaji ya umati katika ukanda huo. Mabalozi hao wa nchi za Kiislamu wamesema kuwa watu wanaopoteza maisha yao katika mashambulio hayo ya kinyama ya Israel ni watoto wadogo, wanawake na raia wa kawaida na kuutaka utawala huo ufungue mara moja vivuko vyote vya Ukanda wa Gaza ili kuruhusu kuingia katika ukanda huo misaada ya dharura ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na madawa na chakula. Taarifa hiyo pia imezitaka jumuiya mbalimbali za kimataifa kufanya kila liwezekanalo kwa madhumuni ya kusimamisha mara moja mabashambulio ya kinyama yanayofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na kuuarifisha utawala huo kuwa utawala wa kivamizi. 342455
captcha