IQNA

Waislamu wa Sydney waandamana kupinga jinai za Israel

12:02 - January 03, 2009
Habari ID: 1726495
Waislamu wa Sydney, Australia wameandamana mjini humo wakilaani jinai na mauaji yanayofanywa na utawala za Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Baada ya swala ya Ijumaa ya jana Waislamu wa Sydney walifanya maandamano wakielekea katika mojawapo na bustani kubwa za mji huo na kulaani mauaji ya umati yanayofanywa dhidi ya wakazi wa Gaza.
Wamesisitiza kuwa vifaru, makombora na mabomu ya Israel hayawezi kuvuruga umoja na mshikamano wa Kiislamu.
Ibrahim Abu Muhammad ambaye ni miongoni mwa viongozi wa jamii ya Waislamu wa Australia alihutubia mjumuiko huo akizitaka nchi za Kimagharibi kuchukua hatua dhidi ya mashambulizi ya Israel na kuwafikisha mahakamani viongozi wa utawala huo kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita. 342464


captcha