IQNA

Haddad Adel:

Wimbi la malalamiko ya Waislamu dhidi ya jinai za Israel litazidisha mzigo wa kimya cha serikali za Kiarabu

12:06 - January 03, 2009
Habari ID: 1726507
Wimbi la maandamano na malalamiko ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya dunia dhidi ya jinai zinazoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza linapaswa kuwa kali zaidi na kuzidisha uzito na gharama za kimya cha serikali za Kiarabu na kuzilazimisha kuchukua hatua.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Utamaduni ya Bunge la Iran Ghulamreza Haddad Adel ambaye pia ameashiria maafa makubwa yanayotekelezwa na Israel katika Ukanda wa Gaza na kusema, Waislamu wanalazimika kutetea haki za wananchi wa Palestina.
Haddad Adel ameashiria kimya cha baadhi ya serikali za Kiarabu mbele ya maafa ya kibinadamu huko Gaza na akasema kuwa, tawala hizo zilikuwa na habari kuhusu njama za Israel na ni muhali kwa utawala huo kutekeleza mashambulizi ya kijeshi huko Gaza bila ya kushirikiana na tawala hizo.
Spika wa zamani wa bunge la Iran amesema kuwa matokeo ya kimya hicho cha serikali za Kiarabu ni kuyumba kwa misingi ya tawala zao na kwamba utendaji wao unazidisha chuki na hasira za Waislamu kote duniani. Amesema kuwa wadhifa wa wananchi na jumuiya mbalimbali mbele ya jinai za Israel huko Gaza ni mkubwa mno. 342449
captcha