Kwa kuendesha mashambulio ya kinyama dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza, utawala wa Israel haulengi tu kuifuta harakati ya Hamas bali umeazimia kufuta sura na utambulisho wa Kiislamu wa Wapalestina na hivyo kuwadhalilisha Waislamu na Waarabu wote.
Hayo yamesemwa na Sheikh Isah Qassim, mkuu wa Mashia wa Bahrain katika Msikiti wa Imam Swadiq (as) huko Manama, mji mkuu wa nchi hiyo. Sheikh Qassim amesema kuwa ni wajibu kwa Waislamu wote kuendelea kufanya maandamano ya kulalamikia mauaji na jinai za uatwala huo dhidi ya Wapalestina wasio na hatia na kulaani kwa kila njia jinai hizo. Amesema kama Wazayuni uwezo mkubwa na msimamo mmoja katika ulimwengu wa Kiarabu, kamwe hawangefanya kiburi cha kutekeleza mauaji ya umati dhidi ya Waarabu wenzao huko Gaza. Amesema, ni jambo la kuaibisha mno kwa baadhi ya Watawala kuzitegemea nchi za Magharibi ambazo zenyewe ni waugaji mkono wakubwa wa utawala haramu wa Israel ili kuulazimisha usimamishe jinai na mauaji ya kinyama unayoyatekeleza dhidi ya wakazi wasio na ulinzi wa Gaza. Ayatullah Sheikh Isah Qassim amesisitiza kwamba, watawala wanaozungumzia suala la kuboresha uhusiano na utawala haramu wa Israel wanapasa kusubiri siku kama hizi za kudhihirishwa utambulisho halisi wa kijinai wa Wazayuni, ambapo unawaua kwa umati ndugu zao wa Palestina huku ulimwengu ukiwa umekaa kimya bila ya kuchukua hatua yoyote ya kukabiliana na jinai hiyo. Ayatullah Isah Qassim amezungumzia umuhimu wa siku hizi za maombolezo ya mwezi mtukufu wa Muharram na kuwataka Mashia watumie vyema ujumbe wa mapambano ya Imam Hussein (as) huko Karbala Iraq, kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano, kusameheana, kufanya mazungumzo na kuishi pamoja kwa amani. 342815