IQNA

Kamati ya kuwaunga mkono watu wa Ghaza yaanzishwa Bahrain

23:46 - January 03, 2009
Habari ID: 1726896
Kamati ya kitaifa ya kuwapa himaya wakazi wa Ghaza imezinduliwa nchini Bahrain kufuatia amri ya mfalme wa nchi hiyo Hamad bin Issa Al Khalifa.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Bahrain GNA, Moustafa as-Sayyid Katibu Mkuu wa Taasisi ya Misaada ya Al Malikia ya Bahrain amesema kuwa: "Kamati ya Kitaifa ya kuwaunga mkono Wapalestina waishio Ghaza imeanza kazi zake chini ya usimamizi wa taasisi ya Al Malikia".
Ameongeza kuwa kamati hiyo kwa ushirikiano wa Hilali Nyekundi ya Bahrain itakusanya misaada ya kibinadamu nchini humo na kuituma kwa wakazi wanaopata masaibu wa Ghaza.
Moustafa as-Sayyid amesema, mwanamfalme Nasir bin Ahmad Al Khalifa ndiye atakayesimamia Kamati ya Kitaifa ya kuwaunga mkono Wapalestina waishio Ghaza na kwamba atafanya juhudi za kukusanya misaada ya kuwasaidia Wapalestina.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya nje wa Bahrain Khalid bin Ahmad Al Khalifa amekutana na Kamati ya Masuala ya Kigeni ya Bunge la nchi hiyo na kutaka hatua za haraka zichukuliwe kuzuia mauaji ya kimbari ya Wapalestina yanayotekelezwa katika hujuma ya kinyama ya Israel dhidi ya Ghaza. Ameitaja hujuma ya Wazayuni kuwa ya kinyama na inayokiuka misingi yote ya kibinadamu. Khalid bin Ahmad Al Khalifa amesema, haki za Wapalestina zitapatikana tu kwa kuundwa nchi huru ya Kipalestina mji wake mkuu ukiwa Bait ul Muqaddas. Aidha waziri huyo wa Bahrain ametoa wito kwa makundi yote ya Kipalestina kudumisha umoja na mshikamano ili yaweze kukabiliana ipasavyo na hujuma za kinyama za Wazayuni. 342895
captcha