Marekani imepinga tena muswada uliowasilishwa na nchi za Kiarabu ukitaka kusitishwa mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza. Baraza la Usalama lilikutana hivi karibuni kujadili mgogoro wa Gaza na mashambulizi ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wasio na hatia wa eneo hilo. Muswada huo uliowasilishwa na Libya kwa niaba ya nchi za Kiarabu, ulieleza wasiwasi mkubwa wa jamii ya kimataifa kuhusu hali ya Gaza hususan baada ya Israel kuanzisha mashambulizi ya nchi kavu katika eneo hilo.
Siku chache zilizopita pia Marekani ilitumia kura ya veto kuzuia hatua yoyote ya kulaaniwa hata kwa maneno matupu mashambulizi na mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya raia wa Palestina.
Katika upande mwingine, Miguel D’Escorto , raia wa Nicaragua ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amekosoa vikali kushindwa Baraza la Usalama kuchukua hatua yoyote ya kusimamisha hujuma ya Israel huko Gaza. Amesema: “Suala hili litapoteza itibari ya Umoja wa Mataifa”. Aidha ameyataja mashambulio ya Israel huko Gaza kuwa ya kinyama na kuzilaumu nchi za Magharibi kwa kuwa na misimamo ya kindumakuwili mbali na kulitimia vibaya Baraza la Uslama kwa maslahi yao.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amenukuliwa akisema kuwa usitishaji vita unapaswa kufikiwa iwapo tu malengo ya Israel huko Ukanda wa Gaza yatafikiwa. 343691