IQNA

Gaza itakuwa medani nyingine ya ushindi wa damu dhidi ya upanga

13:18 - January 05, 2009
Habari ID: 1727539
Kumtegemea Mwenyezi Mungu, mantiki ya haki, irada ya mujahidina, ukakamavu na uendelevu ni mambo yanayoambatana na ushindi na Gaza kwa mara nyingine itakuwa medani ya ushindi wa damu dhidi ya upanga. Hayo yamesemwa na Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
Akizungumza katika majlisi ya maombolezo ya Imam Hussein (as) mjini Beirut Lebanon, Sayyid Nasrullah aliongeza kuwa: “Kinachotokea hivi sasa huko Gaza ni hujuma dhidi ya eneo hilo. Haya ni mambo yaliyojiri wakati Wazayuni walipovamia Lebanon (katika vita vya siku 33 mwaka 2006). Hujuma ya Gaza inatokana na fursa na idhini iliyopata Israel kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa”.
“Ndugu zetu huko Palestina wanaelewa vyema yanayojiri na nukta ya msingi katika vita hivi ni kumpa adui kipigo. Hujuma hii haitaenea maeneo mengine ya Palestina maadamu harakati ya mapambano ipo”, amesema Sayyid Nasrullah.
Kiongozi wa Hizbullah ametoa wito wa kuwepo ufungamano na makundi yanayopambana Palestina na kutuma misaada kwa wapiganaji jihadi ili wapate ushindi. Sayyid Nasrullah amesema kile kinachojiri Gaza ni kutetea ardhi za Palestina pamoja na matukufu ya Kiislamu. 343667

captcha