IQNA

Misri imewataka Wazayuni kufanya mashambulizi ya nchi kavu huko Gaza na kudhibiti kivuko cha Rafah

11:51 - January 05, 2009
Habari ID: 1727782
Vyombo vya kuaminika vya nchi za Kiarabu vimeashiria ushirikiano wa viongozi wa Cairo na Tel Aviv na kufichua kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel na Misri zimepanga mikakati ya pamoja ya kukaliwa kwa mabavu eneo la mpakani mwa Gaza na Misri mkabala wa kivuko cha Rafah ili Cairo ijiondoe chini ya mashinikizo makali ya lawama za kufunga kivuko hicho mbele ya Wapalestina.
Vyombo vya kidiplomasia vya nchi za Kiarabu za kandokando ya Ghuba ya Uajemi vimetangaza kuwa, jeshi la adui Mzayuni linafanya jitihada za kuukalia kwa mabavu ukanda wa mpakani mwa Gaza na Misri kupitia mashambulizi yake ya nchi kavu huko Gaza. Vyombo hivyo vimeongeza kuwa uamuzi wa kukaliwa kwa mabavu ukanda wa kandokando ya kivuko cha Rafah ulichukuliwa katika mashauriano yaliyofanyika kati ya viongozi wa Israel na Misri. Vimeongeza kuwa lengo la hatua hiyo ni kumuondoa Rais Hosni Mubarak chini ya mashinikizo makali yanayomlaumu kwa kufunga kivuko hicho mbele ya wananchi wa Palestina wanaokabiliwa na mzingiro mkali wa Wazayuni.
Vyombo hivyo vimesema kuwa, iwapo ukanda wa mpakani wa Rafah utakaliwa kwa mabavu, hatua hiyo itapunguza mashinikizo yanayomkabili Rais wa Misri, na eneo zima la Gaza litakaliwa kwa mabavu kikamilifu na majeshi ya Israel.
Wiki iliyopita duru za Ulaya zilifichua kwamba nchi tatu za Misri, Saudi Arabia na Jordan zimeshirikiana na adui Mzayuni na kuidhinisha mashambulizi ya kijeshi ya utawala haramu wa Israel dhidi Gaza kwa shabaha ya kutokomeza harakati ya Hamas.
Mashambulizi ya kinyama yanayoendelea kufanywa na jeshi la utawala katili wa Israel tangu siku kumi zilizopita yamesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 520 na kujeruhi wengine zaidi ya 2500. 811601
captcha