Kufuatia hujuma ya utawala haramu wa Israel huko Gaza na kushindwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa azimio la kuushurutisha utawala huo kusitisha jinai zake, taasisi hiyo ya kimataifa imepoteza itibari yake.
Walimwengu wengi walikuwa waskisubiri baraza hilo kuchukua uamuzi wa kuzuia maafa zaidi huku Gaza. Hata hivyo kama kawaida yake, Marekani ilitumia kura ya turufu au veto kuzuia azimio lolote dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Kwa miongo kadhaa sasa Marekani imekuwa ikupinga hatua yoyote kali kuchukuliwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya jinai za utawala ghasibu wa Israel huko Palestina. Msimamo huo wa Marekani umemkasirisha Miguel D’Escorto Mwenyekiti wa Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa ambaye amekosoa vikali kushindwa Baraza la Usalama kuchukua hatua yoyote ya kusimamisha jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza. Amesema suala hilo limeufanya Umoja wa Mataifa upoteze itibari yake.
Wakati huo huo serikali ya Uswisi imetoa taarifa ikilaani wimbi jipya la uvamizi wa jeshi la Israel huko Gaza. Kwa mujibu wa Ukurasa wa intaneti wa swissinfo.ch, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uswisi imeutaka utawala wa Israel kusitisha mara moja hujuma yake huko Gaza. Aidha Uswisi imelalamikia vikali hatua ya viongozi wa Israel ya kuzuia madaktari wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu kuingia Gaza kuwatibu mejeruhi.
Kufuatia kushadidi ukatili wa Israel huko Gaza, balozi wa Utawala wa Kizayuni huko Geneva ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo na kukabidhiwa malalamiko makali ya wakuu wa Uswisi kuhusiana na hujuma hiyo mpya ya Israel huko Gaza na kutakiwa kufikisha malamiko hayo kwa watawala wa Tel Aviv. 344313