Taarifa iliyotolewa na baraza la Kiislamu la Nigeria imesema kuwa baraza hilo linalaani vikali mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.
Baraza hilo limeyataka mataifa yote duniani, Umoja wa Mataifa na umma wa Kiislamu kulaani jinai za kigaidi za utawala wa Kizayuni ambazo zinahatarisha mustakbali wa dunia na tayari zimeua mamia ya wanadamu wasiokua na hatia yoyote.
Taarifa ya Baraza la Kiislamu la Nigeria ambayo imesomwa katika radio ya taifa ya nchi hiyo, imewataka vijana wote wa Kiislamu kushikamana na taifa la Palestina katika kipindi hiki nyeti na hatari. Vilevile imeyataka mataifa yote na Baraza la Usalama kuchukua msimamo wa wazi na wa kiadilifu kuhusu mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.
Baraza hilo pia limeitaka jamii ya kimataifa kufanya jitihada za kuunda dola huru la Palestina. 344818