Mawakili wa mjini London Uingereza, wamemtaka mwendesha-mashtaka mkuu wa nchi hiyo kutoa kibali cha kutiwa nguvuni baadhi ya watawala wa utawala haramu wa Israel na Misri kwa kuhusika na vitendo vya jinai za kivita dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.
Katika taarifa waliyotoa leo Jumamosi, mawakili hao wametaka kufikishwa mahakamani Shimon Peres, Tzipi Livni Ehud Olmert na Ehud Barak, Rais, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri Mkuu na Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel kwa utaratibu kutokana na kuhusiaka kwao na jinai za kivita dhidi ya wakazi wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza. Vilevile wametaka kutiwa nguvuni Ahmad Nadhif, Waziri Mkuu na Ahmad Abul Ghait, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri kwa ushirikiano wao na utawala haramu wa Israel katika kuwaua kinyama Wapalestina na pia kufunga kivuko cha Rafah na hivyo kuzuia misaada ya dharura ya kibinadamu kuwafikia wananchi wanaoteseka na kuuawa kinyama katika Ukanda wa Gaza.
Mawakili hao pia wanasisitiza kwamba, katika kipindi cha wiki mbili cha mashambulio yake ya kinyama katika Ukanda wa Gaza, utawala haramu wa Israel umekuwa ukikiuka sheria za kimataifa na kukanyaga wazi haki za binadamu kwa kuwaua kwa umati watu wasio na hatia wala ulinzi katika ukanda huo. 345627