IQNA

Matokeo ya vita vya siku 33 vya Lebanon yanaisubiri Israel

15:28 - January 10, 2009
Habari ID: 1729011
Kuendelea kwa mashambulio ya kinyama ya utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia huko katika Ukanda wa Gaza hakutadhoofisha mapambano ya Wapalestina wakazi wa ukanda huo, bali utawala huo wa Kizayuni, kama ilivyokuwa katika vita vyake vya kichokozi vya siku 33 nchini Lebanon, unapasa kusubiri kupata pigo la kufedhehesha kutoka kwa wanamapambano wa Palestina.
Hayo yamesemmwa na Hujjatul Islam wal Muslimeen, Sadruddin Qubanchi, Imam wa Swala ya Ijumaa ya mji mtakatifu wa Najaf. Imam huyo amehoji, katika hali ambayo wananchi wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza wanashambuliwa kinyama na utawala haramu wa Israel, ni vipi jamii ya kimataifa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimeamua kukaa kimya na kutosema lolote kuhusiana na mauaji hayo ya umati? Amesema, kwa kimya chake hicho, Baraza la Usalama limetoa fursa kwa utawala haramu wa Israel uendelee kutekeleza mauaji ya umati dhidi ya wakazi wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza na wakati huohuo kukandamiza na kuifuta kabisa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas.
Sayyid Sadruddin Qubanchi ameongeza kuwa, mauaji ya umati yanayoendeshwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza yanakiuka misingi na mafundisho ya dini zote za mbinguni na kuwa ni vita vya wazi dhidi ya Waislamu. Imam huyo wa Swala ya Ijumaa ya mjini Najaf amesema kuwa, mauaji ya Gaza ni mkasa mkubwa wa kibinadamu na kuwataka viongozi wa Kiarabu na Kiislamu kufanya juhudi za kusimamisha mara moja jinai hizo za kinyama za utawala wa Israel katika ukanda huo. 345586
captcha