Dua maalumu ya kuwaombea wahanga wa mashambulio hayo imefanyika katika misikiti yote ya Ijumaa katika nchi hiyo pana.
Sheikh Damir Gizatolin, Naibu Mkuu wa Baraza la Mamufti wa Russia amesema kuwa, shughuli hiyo maalumu ya kuwaombea dua Wapalestina wanaoteseka na kuuawa kwa umati na utawala haramu wa Israel itaendelea kufanywa kila Ijumaa hadi mashambulio hayo ya kinyama yatakapokomeshwa na utawala huo. Amesema, Waislamu hawawezi kukaa kitako na kunyamazia jinai hiyo kubwa ambapo utawala haramu wa Israel unawaua kinyama watoto, wazee na wanawake wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
Waislamu wa Russia wanasisiza kwamba wataendelea kuwaombea dua wenzao wa Mashariki ya Kati na hasa Wapalestina wa Ukanda wa Gaza ili maadui wa Kizayuni wasimamishe mashambulio yao ya kinyama dhidi yao.
Mashambulio hayo ya kijinai yanayotekelezwa na utawaka haramu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza tokea tarehe 27 Disemba hadi sasa yamepelekea raia karibu 900 kupoteza maisha yao na wengine zaidi ya 3500 kujeruhiwa. 8710210060