IQNA

Maulamaa wa Kiislamu Ache wako tayari kupigana jihadi Palestina

10:26 - January 11, 2009
Habari ID: 1729281
Maulamaa na wanafunzi wa Kiislamu wa jimbo la Ache nchini Indonesia wametangaza kuwa wako tayari kwenda kupigana vita vya jihadi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Gazeti la Jakarta Post limeandika kuwa, maelfu ya maulamaa na wanafunzi wa Kiislamu wa Ache Indonesia wamekusanyika katika msikiti mkuu wa jamaa wa mji huo wakiwaombea dua Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya kinyama ya utawala ghasibu wa Israel huko Gaza na kutangaza kuwa iwapo serikali itaruhusu, wako tayari kwenda kupigana jihadi huko Palestina.
Viongozi waliohutubia mkusanyiko huo wamelaani jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza na kuashiria kuwa wanawake na watoto wadogo ndiyo wahanga halisi wa mashambulizi hayo. 345913

captcha