Taarifa iliyotolewa na wanazuoni wa Morocco imesema: Hatua ya vijana wa Morocco ya kushambulia na kuvuruga mitandao na vituo cha upashaji habari vya Israel inaonyesha hasira na chuki ya vijana wa Kiislamu dhidi ya Wazayuni na upinzani wa vijana hao dhidi ya mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na utawala huo huko Gaza.
Sheikh Bin Salim Bahisham ambaye ni mwanachama wa Jumuiya ya Maulamaa wa Morocco amesema kuwa kuna mbinu mbalimbali za kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuwatetea wananchi wa Gaza na kwamba mashambulizi dhidi ya vituo vya intaneti vya Israel ni hatua sahihi na ya kupongezwa katika uwanja wa jihadi ya elektroniki.
Sheikh Bahisham ameongeza kuwa, kuvuruga vituo vya intaneti vya upashaji habari vya Israel kunawashinikiza Wazayuni na kulenga taasisi zao za mawasiliano.
Kundi moja la vijana wa Morocco linaloitwa "Morocco Snipers" limeharibu vituo 80 maarufu vya intaneti vya Israel katika kipindi cha wiki iliyopita na kubandika picha za mauaji ya raia wasiokuwa na hatia waliouawa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza katika kurasa za mitandao hiyo. 346514