Naomi Klein, mwandishi wa Uingereza na mmoja wa wapigania haki za binadamu nchini humo amesema katika makala moja aliyoandika hivi karibuni katika gazeti la Guardian kwamba, njia bora zaidi ya kumaliza uvamizi na kukaliwa kwa mabavu ardhi za Wapalestina na utawala haramu wa Israel, ni utawala huo kuwekewa vikwazo vya pande zote vya kimataifa.
Naomi Klein ameandika katika makala hiyo kwamba, makumi ya wasanii na watafiti wa Kiyahudi wamezitumia baraua balozi za kigeni katika mji wa Tel Aviv wakizitaka zitoe mashinikizo dhidi ya Utawala haramu wa Israel ili usimamishe mauaji yake ya umati dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
Bi Klein amesisitiza kwamba, vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa ndiyo njia bora zaidi ya kuulazimisha utawala haramu wa Israel usimamishe mara moja mashambulio yake dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
Amesema, tokea mwaka 2006 hadi sasa utawala ghasibu wa Israel umetekeleza jinai na uhalifu mkubwa kwa kujenga vitongaji vya Mayahudi katika ardhi za Wapalestina, vita vya kichokozi dhidi ya Hizbullah ya Lebanon, na hivi sasa mashambulio ya kinyama dhidi ya watu wasio na hatia wa Gaza.
Mwandishi huyo amesema mwishoni mwa makala yake katika gazati la Guardian kwamba, kukatwa uhusiano wa kidiplomasia na Israel kutaupoozesha utawala huo ambao unategemea biashara ya kigeni na kwamba hatua hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kuushinikiza usimamishe mara moja mashambulio yake hayo ya kinyama dhidi ya Wapalestina wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza. 346861