Kwa mujibu wa shirika la habari la Saphirnews, jumuiya hiyo imetoa wito kwa vyombo vyote vya habari vya Ufaransa kulaani jinai za Wazayuni katika Ukanda wa Gaza na kukosoa matamsi ya baadhi ya wakuu wa kisiasa na wamiliki wa vyombo habari nchini Ufaransa kuhusu matukio ya Gaza.
Vijana wa Ufaransa wametaka vita visivyo na mlingano huko Gaza kusitishwa mara moja. Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Vijana wa Ufaransa imesema kuwa: “Wanapaswa kuona aibu wale ambao wamewazingira watu milioni moja na nusu wasio na hatia na baada ya hapo kuwashambulia kupitia angani na nchi kavu. Wanapaswa kuona aibu watu ambao huhadaa ulimwengu kuwa eti vita hivi ni dhidi ya Hamas na si dhidi ya Wapalestina!".
Jumuiya ya Vijana wa Ufaransa imekosa kimya cha viongozi wa nchi hiyo na jumuiya za kimataifa mbele ya jinai za Israel. Jumuiya hiyo imehoji: “Ni vipi tunanyamaza kimya wakati majengo ya raia, shule na mahospitali yanaharibiwa katika hujuma isiyo na huruma ya makombora ya utawala wa Kizayuni? Ziko wapi sauti ambazo zinatosheka kwa kutoa matamshi ya kawaida ya kulaani?
Jumuiya hiyo imesema, ni jukumu la vijana wa Ufaransa kutumua njia zote za kisheria na kwa utulivu, kulaani jinai za Israel. Aidha vijana Waislamu Ufaransa wamewaunga mkono watu wanaodhulumiwa Palestina na kutoa wito kwa raia wote wa Ufaransa kufanya kila wawezalo kuhakikisha jinai za Israel huko Gaza zinakomeshwa mara moja. 347700