Waandamanaji hao wa Kiyahudi wametangaza kuwa, iwapo mashambulizi hayo hayatasitishwa haraka iwezekanavyo idadi ya watu waliouawa na kujeruhiwa kutoka pande zote mbili itaongezeka zaidi.
Hadi sasa zaidi ya Wapalestina 900 wameuawa shahidi na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi hayo.
Kundi la Mayahudi lililotayarisha maandamano hayo limetangaza kwamba: Waandamanaji hao raia wa Marekani wanaamini kuwa kuendelea kwa mashambulizi ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza kutakuwa na maslahi kwa Marekani na si kwa utawala wa Israel.
Kundi hilo limewataka viongozi wa Marekani kufanya juhudi za kutatua kwa amani na kwa njia za kidiplomasia mgogoro wa vita kati ya Israel na Waarabu na kutahadharisha kwamba: Mashambulizi ya Gaza yamezidisha chuki za walimwengu dhidi ya Israel na waitifaki wake ikiwemo Marekani na kuchafua sura zao.
Israel imeendelea kupuuza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa mashambulizi dhidi ya raia wa Gaza. 347461