IQNA

Qur’ani Tukufu, Kitabu cha pili kuuzwa kwa wingi katika maonyesho ya vitabu ya India

9:59 - January 15, 2009
Habari ID: 1731171
Qur’ani Tukufu imechukua nafasi ya pili ya mauzo ya vitabu katika maonyesho ya vitabu nchini India.
Katika maonyesho hayo yaliyofanyika katika mji wa Nagpur, katika jimbo la Maharashtra, mauzo ya Qur’ani ambayo imetarjumiwa kwa lugha tofauti, yamechukua nafasi ya pili baada ya kitabu cha Ramyan ambacho ni kitabu cha Kihindi kinachozungumzia masuala ya hamasa. Watu wapatao laki nne waliyatembelea maonyesho hayo ya siku 10 ambapo zaidi ya vitabu milioni moja tofauti vilionyeshwa.
India ina zaidi ya Waislamu milioni 150, idadi ambayo ni asilimia 14 ya wananchi wote wa nchi hiyo. 348107
captcha