Gazeti la Imarati la al-Khalij limemnukuu Abdallah Abdul Jabbar, mkuu wa ofisi ya masuala ya uhubiri ya idara hiyo akisema kuwa, CD hiyo inajumuisha sauti za wasomaji bora na mashuhuri kama vile Abul Ainein Shesha, Abdul Basit, Ahmad Nueina, Mustafa Ismail, Abdul Fatah Sha’shai, Muhammad Rafat, Ali Mahmoud, Taha al-Fashni, Kamal Yusuf na Muhammad an-Nur. Amesema katika hatua ya kwanza, tayari nuskha 3000 za CD hiyo zimekwishasambazwa miongoni mwa walimu wa vituo vya Kiislamu na Qur’ani, wahubiri na wanachuo wa vituo vya kusoma na kuhifadhi Qur’ani kote nchini Imarati.
Abdul Jabbar, amesisitiza kwamba, namna saba ya usomaji Qur,ani umebainishwa katika CD hiyo kupitia wasomaji hao wa Qur’ani katika ulimwengu wa Kiislamu, na kwamba CD hiyo itatumika katika mafunzo ya juu na kitaalamu ya Qur’ani kwa wanafunzi. 348131