Wataalamu 18 waandamizi wa Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa wametoa taarifa wakitangaza kuwa, jinai za Israel katika eneo la Gaza na utumiaji wa mabomu yaliyopigwa marufu kimataifa utakuwa na taathira nyingi mbaya za kinafsi kwa vizazi vijavyo vya Ukanda wa Gaza.
Taarifa hiyo imesema: Israel inalenga shule na mahospitali mengi ya Ukanda wa Gaza na kukiuka sheria za kimataifa kwa kuwashambulia watoto wadogo na raia wa kawaida wakati wa vita.
Taarifa ya wataalamu wa ngazi za juu wa Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa tangu Israel ianze mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Gaza zaidi ya watoto 300 wameuawa na kwamba watoto wa eneo hilo wanakabiliwa na matatizo makubwa kupata misaada ya kibinadamu na mahitaji ya kimsingi ya kimaisha.
Taarifa hiyo imeashiria mashambulizi yaliyofanya na jeshi la Israel dhidi ya shule ya al Fakhoora inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza na kusema: Wanafunzi 43 waliuawa katika shambulizi hilo na makumi ya wengi kujeruhiwa. 348161