Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kuwa Gilles Bernheim ameashiria mchango mkubwa wa viongozi wa kidini katika kuimarisha amani ya kimataifa na akasema: Viongozi wa dini za Kiislamu, Kikristo na Kiyahudi nchini Ufaransa wanapaswa kufanya jitihada za kurejesha amani Mashariki ya Kati hususan Ukanda wa Gaza.
Kiongozi wa kidini wa Mayahudi wa Ufaransa amesema kuwa, kazi ya viongozi wa kidini ni kufikisha ujumbe wa amani na kwamba ana matumaini mgogoro wa Gaza hautakuwa mgogoro kati ya wafuasi wa dini tofauti nchini Ufaransa. 348183