Huku akisema kuwa nchi za Kiarabu hazina uwezo wa kukabiliana kijeshi na utawala haramu wa Israel, Abdulqadir Hajjar, balozi wa Algeria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa, njia na silaha bora zaidi ya kukabiliana na utawala huo ni kupitia vikwazo vya mafuta.
Akizungumza na mtandao wa televisheni ya al-Jazeera, Hajjar amesisitiza kwamba, vikwazo vya kiuchumi na kutopelekwa mafuta ya nchi za Kiarabu huko Israel, ndiyo njia bora na ya pekee ya nchi hizo kushinikiza na kuufanya utawala huo usimamishe mauaji ya umati na jinai zake huko katika Ukanda wa Gaza. Amesema kuwa iwapo wakuu wa nchi za Kiarabu katika kikao chao huko Doha Qatar na kile kingine cha kiuchumi kinachotazamiwa kufanyika nchini Kuwait watachukua uamuzi wa kusimamisha na kufunga akaunti zao za kifedha nchini Marekani, bila shaka utawala ghasibu wa Israel utasimamisha mashambulio yake huko Gaza katika kipindi cha masaa 12.
Abdulqadir Hajjar amesisitiza kwamba, iwapo watawala wa nchi za Kiarabu watachukua hatua ya kuuwekea utawala haramu wa Israel vikwazo vya kiuchumi na nishati, bila shaka utawala huo utalazimika kubadili siasa zake dhidi ya Wapalestina na Waarabu kwa ujumla. 348988