Matini ya Qur'ani hiyo ya dijitali imeandikwa kwa hati na mwandiko wa Othman Twaha na kiraa yake imesomwa na Imamu wa msikiti mtukufu wa Makka Sheikh Mahir al Muayqali ambaye ni mmoja wa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani.
Qur'ani hiyo ya dijitali pia ina tarjumi ya lugha saba za Qur'ani Tukufu ambazo ni Kiingireza, Kifaransa, Kiholanzi, Kituruki, Kiindonesia, Malayo na Urdu.
Qur'ani hiyo ya dijitali pia ina adhana, dua za Kiislamu na majina matukufu ya Mwenyezi Mungu ya Asmaul Husna, dua ya kuhitimisha Qu'ani, nyakati za swala katika nchi mbalimbali duniani, alama ya kuonyesha kibla na saa.
Sifa nyingine za chombo hicho cha Qur'ani ya dijitali ni kwamba ni chepesi na kinaweza kuwekwa mfukoni kirahisi. Vilevile kina sauti na picha nzuri na kinauzwa kwa bei nafuu.
Kampuni ya ENMAC ndio kituo kikuu cha kuzalisha zana za dijitali za Kiislamu. Ofisi kuu ya kampuni hiyo iko katika mji wa Shenzhen katika mkoa wa Guangdong kusini mashariki mwa China.
Kampuni hiyo ina matawi katika miji kadhaa kama vile Hong Kong, Dubai, Lahore na Cape Town Afrika Kusini. 349630