Hayo yametangazwa na Sheikh Hamad bin Jassim bin Jabr Aal Thani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar ambaye pia ni Waziri Mkuu wa nchi hiyo ya kifalme na kuongeza kuwa Qatar ni nchi ya Kiarabu ambayo imechukizwa mno na kulaani mashambulio ya kinyama ambayo yamefanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia huko katika Ukanda wa Gaza.
Sheikh Hamad bin Jassim amesema, hatua hiyo imechukuliwa na serikali ya Qatar kama alama ya kulalamikia mashambulio ya kinyama ambayo yamefanywa na utawala huo ghasibu dhidi ya watu wasio na ulinzi katika ukanda huo. Sheikh Hamad vilevile amesema kuwa nchi hiyo daima imekuwa ikifanya juhudi za kutatua mgogoro wa Palestina na kusimamisha mashambulio ya kinyama dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza, lakini bila ya mafanikio. 350418