IQNA

Bunge la Yemen lapitisha muswada unaopiga marufuku uhusiano na Israel

11:27 - January 22, 2009
Habari ID: 1734276
Bunge la Yemen sambamba na kutangaza mshikamano wake na watu wa Ukanda wa Gaza limepitisha muswada wa sheria inayopiga marufuku uhusiano wowote na utawala haramu wa Israel katika nyanja za kisiasa, kibiashara na kitamaduni.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Aljazeera.net, Muhammad Al Hezami, Mbunge wa mrengo wa Al Islah katika Bunge la Yemen amesema: “Kwa mujibu wa sheria hiyo, taasisi yoyote ya Yemen itakayojaribu kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel itaadhibiwa”.
“Sheria hiyo ina vipengee 10 ambayvo vinapiga marufuku kabisa muamala na uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kitamaduni na utawala wa Kizayuni. Kufungua ofisi ya kibiasahra na kisiasa ya Israel nchini Yemen au kutia saini mikataba ya ushirikiano na taasisi za Israel kutahesabiwa kuwa ni sawa na kushirikiana moja kwa moja na unyama unaotekelezwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina”, amesema mbunge huyo wa Yemen.
Muhammad Al Hezami amebainisha kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo, kuwa na muamala na Israel au kushiriki kwa anwani yoyote katika kikao chochote kinachojadili suala la kuwapokonya Wapalestina ardhi zao kutahesabiwa kuwa jinai kubwa na yeyote atakayekiuka sheria ataadhibiwa vikali na hata adhabu ya kifo yaweza kutekelezwa dhidi yake.
Mjumbe huyo wa mrengo wa Al Islah katika bunge la Yemen amesema, mtu yeyote atakayepatikana na hati ya kujaribu kuanzisha uhusiano wa kawaida wa kisiasa, kitamaduni na kibiashara na Irael atafungwa kifungo cha hadi miaka 10 jela mbali na kupigwa marufuku kushikilia wadhifa serikalini katika maisha yake yote.
Muhamad Al Hezami ameashiria namna suala la kuwa na uhusaino wa kwaida na Israel lilivyoleta hitilafu na ufa miongoni mwa nchi za Kiislamu na Kiarabu na kusisitiza kuwa: “Ardhi za Wapalestina ni za Waislamu wote na nchi za Kiislamu na Kiarabu hazina haki hata kidogo kulegeza msimamo kwa maslahi ya adui Mzayuni. Serikali yoyote itakayoanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni kwa jina la eti ‘amani’ inapaswa kuadhibiwa”. 352050




captcha