Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Morocco MAP, madaktari hao wanajumuisha wapasuaji, wataalamu wa magonjwa ya watoto, wataalamu wa ubongo n.k na wanatazamiwa kuondoka mji mkuu wa nchi hiyo Rabat mwishoni mwa wiki na wakielekea Palestina.
Ujumbe wa madaktari wa Morocco unashirikiana na kamati ya Kiislamu ya Quds kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Gaza waliojeruhiwa katika hujuma ya kinyama ya utawala haramu wa Israel kwa muda wa siku 22.
Katika kipindi hicho cha vita dhidi ya raia wa Gaza, serikali ya Morocco ilituma tani 234 za madawa na chakula kwa wakazi wa eneo hilo. 352178