Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Walmuslimin Abulfat'h Da'wati, mtafiti wa masuala ya kidini wa Iran ambaye ameongeza kuwa, moto wa ubeberu wa Israel katika ulimwengu wa Kiislamu hautazima bila ya viongozi wa utawala huo wa Kizayuni kuzima sauti za kupigania uhuru za Waislamu.
Hujjatul Islam Da'wati amesema kuwa, Wazayuni hawatatosheka na mauaji waliyofanya Ukanda wa Gaza bali baada ya jinai za Gaza utawala huo ghasibu utazishambulia kinyama Misri na ardhi nyingine za Kiislamu kwa shabaha ya kutekeleza malengo yake maovu.
Mtafiti huyo wa masuala ya kidini amesema, mgafala wa umma wa Kiislamu umepelekea kutokea jinai za kinyama za Israel huko Gaza na katika kivuli cha mgafala huo ulimwengu wa Kiislamu umekumbwa na msiba mkubwa. Amesisitiza kwamba kujiondoa kwenye masaibu hayo kunawezekana tu kupitia njia ya kumjua adui, kuwa na umoja na mapambano ya Waislamu.
Abulfat'h amesema, kwa sasa umma wa Kiislamu unapaswa kulinda umoja na mshikamano wake kuliko wakati wowote mwingine na kufanya jitihada za kung'oa kabisa donda hilo la kansa (Israel) na kukomesha vita vya msalaba vinavyoendeshwa na Wazayuni. 351705