Kwa mujibu wa gazeti la Peninsula, katika kikao hicho cha siku nne, mawaziri hao pia watachunguza suala la Palestina.
Kuhusiana na suala la televisheni hiyo ya satalaiti, mawaziri hao wamesema kuwa hilo litakuwa ni jukwaa la Waislamu ulimwenguni kutoa maoni na mitazamo yao kuhusiana na masuala mbalimbali yanayowahusu.
Kuimarishwa idara ya habari na mawasiliano ya OIC, kuimarishwa shirika la habari la umoja huo (IINA) na taasisi ya huduma na maelezo ya nchi za Kiislamu, kuanzishwa kamati ya kudumu kwa ajili ya kuimarisha utamaduni na maelezo na hatimaye kupitishwa kwa bajeti ya kuunganishwa mfumo wa kimataifa wa dijitali ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika kikao hicho. 353772