IQNA

Hamas yaunda kamati ya kuchunguza jinai za kivita za utawala wa Israel

13:39 - January 26, 2009
Habari ID: 1735988
Serikali halali ya Palestina inayoongozwa na chama cha Hamas imeunda kamati itakayochunguza jinai zilizotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha siku 22 za mashambulio yake ya kinyama dhidi ya wakazi wasio na hatia wa ukanda huo.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Hayaat linalochapishwa mjini London Uingereza, Muhammad Faraj al-Ghaul, Waziri wa Sheria wa serikali hiyo amesema kuwa kamati hiyo itasimamiwa na Waziri Mkuu Haniyya na viongozi wengine wa ngazi za juu wa serikali hiyo. Amesema lengo la kuundwa kamati hiyo ni kuchunguza kwa kina jinai zilizotekelezwa katika ukanda wa Gaza na utawala haramu wa Israel katika kipindi cha mashambulio yake dhidi ya watu wasio na hatia, na hatimaye kuwafikisha watawala husika wa mauaji hayo ya umati katika mahakama za kieneo na pia Mahakama ya Kimataifa wa Jinai ICC iliyoko huko The Hague.
Waziri al-Ghaul amesema kuwa watawala wa kisiasa na kijeshi wa utawala wa Israel wametekeleza mauaji na holocaust kubwa zaidi katika historia dhidi ya Wapalestina wakazi wa Ukanda wa Gaza, na kuyataka mashirika ya kieneo na kimataifa ya kutetea haki za binadamu na ya kisheria kufuatilia kwa karibu suala la kufikishwa mahakamani watawala wa Kizayuni waliohusika na mauaji hayo ya umati dhidi ya watu wasio na hatia.
Waziri huyo amewataja Wazayuni hao makatili kuwa Manazi wa zama hizi na kuzitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kuimarisha umoja kwa ajili ya kukabiliana na hujuma za mara kwa mara na za kinyama zinazotekelezwa na utawala huo dhidi ya raia wasio na hatia na pia kufanya juhudi za kufikiwa malengo matukufu ya taifa la Palestina. 353777
captcha