IQNA

Kutengenezwa filamu ya matukio ya kweli (documentary) kuhusiana na jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza

13:42 - January 27, 2009
Habari ID: 1736443
Madaktari walioshuhudia unyama wa utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia katika kipindi cha siku 22 za mashambulio ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza wamesema huko Cairo Misri kwamba, watatengeneza filamu ya matukio ya kweli (documentary) ili kuwafahamisha walimwengu hali halisi ya jinai zilizotekelezwa na utawala huo dhidi ya watu wasio na ulinzi na hasa watoto na wanawake katika ukanda huo.
Wakizungumza na waandishi habari huko Cairo, madaktari hao wamesema kuwa wameazimia kuwaonyesha walimwengu matukio na janga halisi la kibinadamu lililotekelezwa na Wazayuni katika ukanda huo.
Muhammad as-Sharii, mmoja wa madaktari hao amesema kuwa, yale aliyoyashuhudia huko Gaza hayajawahi kushuhudiwa katika kipindi chote cha historia ya mwanadamu.
Huku akionyesha picha za kutisha za wahanga wa mashambulio hayo ya kinyama, Daktari huyo ambaye alikuwa mjini Khan Yunis tokea kuanza kwa mashambulio hayo, amesema kwamba mambo aliyoyashuhudia kuhusiana na janga hilo yalifanana na filamu za kutisha kuliko hali halisi ya mambo.
Rashid Imam, daktari mwingine aliyekwenda huko kuwasaidia wananchi wa Palestina, anasisitiza kwamba hakuna shaka yoyote kwamba, utawala haramu wa Israel ulitumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa katika mashambulio yake hayo dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza. Madaktari hao wamesema kuwa Israel ilitumia katika hujuma yake hiyo ya kijinai silaha ambazo zilikuwa zikikata miili ya wahanga katika vipande vidogovidogo. Madaktari hao wana lengo la kushirikiana na Jumba la Makumbusho la Holocaust ya Wapalestina, ambalo ni jumba la maonyesho lisilo na ukweli wa dhahiri lakini linasimulia ukweli halisi wa mambo, kwa ajili ya kuwafahamisha walimwengu jinai zilizotekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia huko Gaza. 354362
captcha