Gazeti la Saudi Arabia la ar-Riyadh limesema kuwa mashindano hayo ambayo yalianza siku ya Jumatatu na yataendelea kwa muda wa siku tano, yanawashirikisha wahifadhi na wasomaji Qur'ani kutoka nchi za Croatia, Bosnia Herzegovina, Uholanzi, Uturuki, Ufaransa, Ubelgiji, Ujerumani, Albania, Serbia, Macedonia, Kosovo, Austria na Montenegro.
Mashindano hayo yatafanyika katika nyanja kadhaa za kuhifadhi Qur'ani nzima, kuhifadhi juzuu 15 na juzuu 5 na hatimaye mashindano yataingia katika nyanja ya usomaji Qur'ani.
Kamati ya marefa wa mashindano hayo itajumuisha walimu hodari na mashuhuri wa Qur'ani katika nchi za Ulaya.
Mufti wa Croatia na wawakilishi wa kidiplomasia wa nchi za Kiislamu katika nchi hiyo, walimu wa Zagreb, wawakilishi wa taasisi na jumuiya za Kiislamu za Croatia pamoja na idadi kadhaa ya wapenzi wa Qur'ani Tukufu wameshiriki katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo. Shereza za kupewa zawadi washindi wa mashindano hayo zitafanyika siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Kituo cha Kiislamu cha Zagreb. 354909