Shirika Rasmi la Habari la Morocco limetangaza kwamba, mashindano hayo yameandaliwa na Baraza la Kielimu na Kiislamu la Morocco barani Ulaya maalumu kwa raia wa Morocco wanaoishi nchini Ubelgiji na pia kwa raia wengine waliovutiwa na mashindano hayo. Mashindano hayo yalianza siku ya Jumapili na kuwashirikisha watu wengi kutika pembe mbalimbali za Ubelgiji.
Samir ad-Dhuhr Balozi wa Morocco nchini Ubelgiji alitoa hotuba katika sherehe za utoaji zawadi kwa washindi wa mashindano hayo na kusisitiza umuhimu wa kuzingatiwa wahifadhi na wasomaji wa Qur'ani pamoja na kuzingatiwa maana ya kitabu hiki kitakatifu cha Mwenyezi Mungu. Amesema kuandaliwa mashindano hayo kunathibitisha umuhimu unaotolewa na Baraza la Kielimu na Kiislamu la Morocco nchini Ubelgiji kwa suala la kuhifadhiwa utambulisho wa Kiislamu wa Wamorocco na pia udharura wa kulindwa misimamo ya wastani ya Kiislamu na kuishi kwa amani na jamii pamoja na tamaduni nyinginezo ulimwenguni.
Muhammad at-Tajkani, mkuu wa baraza lililotajwa amesema kuwa mwaka ujao litashirikiana na Taasisi ya Qur'ani ya al-Hassan at-Thani kwa ajili ya kuandaa mashindano ya kuhifadhi na tajweed ya Qur'ani Tukufu katika bara zima la Ulaya.
Washindi wa mashindano hayo walitunukiwa zawadi nono za fedha na loho za shukrani. Maimamu wa misikiti na wahubiri wa vituo vya Kiislamu vya Morocco nchini Ubelgiji pia walipewa zawadi katika sherehe hizo. 354925