IQNA

Nchi za Ulaya haziwezi kusaidia ujenzi mpya wa Gaza

15:20 - January 28, 2009
Habari ID: 1737070
Msemaji wa Idara ya Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Ulaya Louis Michel amesema kuwa, nchi za Umoja wa Ulaya hazina uwezo wa kutoa misaada kwa ajili ya ujenzi mpya wa Gaza kutokana na mgogoro kiuchumi duniani.
Kwa mujibu wa ukurasa wa intaneti wa Arab Online, Michel ambaye Jumatatu iliyopita alitembelea eneo la Ukanda wa Gaza amesema kuwa: ‘Katika hujuma ya Wazayuni dhidi ya Gaza miundo mbinu ya eneo hilo iliharibiwa na kunahitajika juhudu za haraka za ujenzi mpya wa eneo hilo.
Aidha amesisitiza juu ya udharura wa kuwepo umoja miongoni mwa makundi ya Kipalestina. Amesema wananchi wa Umoja wa Ulaya hawana matumaini sana kuhusu ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza kutokana na kuwa kuna uwezekano utawala haramu wa Israel ukashambulia tena eneo la Gaza!
Louis Michel amesema kuwa amewataka wakuu wa utawala wa Kizayuni kuheshimu usitishaji vita daima na vile vile kufungua tena vivuko vya Gaza ili kuwezesha misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo la Palestina.
Afisa huyo mwandamizi wa Umoja wa Ulaya vile vile ameulaumu utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kutoheshimu sheria za kimataifa za haki za binadamu na akasema: “ Vikosi vya Israel viliwalenga raia wengi wakiwemo wanawake na watoto katika mashambulizi ya Gaza”. 355117
captcha