Kwa mujibu wa ukurasa wa intaneti wa Al Manar, Muhammad Husseini Mkuu Idara ya Habari katika Kituo cha Opera mjini Cairo amesema: “Tamasha hiyo ya kimataifa ni katika mipango ya Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Misri kwa ajili ya kusaidia ujenzi mpya wa Gaza. Pato la tamasha hiyo litatumika kuwasaidia watu wa Ukanda wa Gaza”.
Amesema wasanii watakaoshiriki ni Ali Othman kutoka Sudan, Fadi Atiya, Hassan Taha na Swahi Al Sman kutoka Syria, Habat Al Qiwas, Mahmoud Darwish, Abubakr Kheira, Abduh Daghr, Atiyya Shrara na Sharif Muhyiddin.
Muhammad Husseini ameongeza kuwa, wanamuziki Waarabu wanaoshiriki katika tamasha hiyo wataimba nyimbo kuhusu jinai za kinyama za utawala wa Kizayuni huko Gaza. Ameongeza kuwa waimbaji wa Misri wametayarisha wimbo kuhusu “Mashahidi wa Gaza. 355691