IQNA

Kuanza ijtimai ya Waislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia nchini Bangladesh

10:27 - February 01, 2009
Habari ID: 1738282
Mkutano wa kila mwaka wa ijtimai ya Waislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia umefunguliwa rasmi katika mji wa Dhaka nchini Bangladesh.
Ijtimai hiyo inayofanyika kwa lengo la kuhuisha misingi ya Uislamu na kueneza amani, inahudhuriwa na Waislamu wasiopungua milioni mbili na zaidi ya elfu sita miongoni mwao wanatoka katika nchi 152.
Katika shughuli hiyo Waislamu hutekeleza kwa pamoja ibada ya swala, kusoma Qur'ani, kuhudhuria vikao vya mawaidha na hotuba za maulamaa wa Kiislamu kuhusu misingi ya Uislamu, amani, ikhlasi, udugu na kusameheana.
Mkusanyiko huo wa ijtimai ndio mkubwa zaidi wa Kiislamu baada ya marasimu ya ibada ya hija.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa karibu asilimia 87 ya jamii yenye watu milioni 150 ya Bangladesh ni Waislamu. 356689
captcha