Kikao hicho ambacho kitahudhuriwa na washairi, wahakiki wa historia na wataalamu wa siasa wa Tajikistan, kitachunguza Mapinduzi ya Miislamu nchini Iran na matunda yake katika nyanja mbalimbali.
Malenga wanne wa mji wa Khujand pia watasoma mashairi kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu katika kikao hicho.
Kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Tajikistan pia kimeahidi kutoa zawadi kwa watu watatu watakaochapisha makala bora magazeti kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na wanafunzi bora 30 wa shule za mji mkuu wa Tajikistan Doshambe watakaoandika makala au kutunga mashairi bora zaidi kuhusu maudhui hiyo.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa Iran imo katika sherehe za kuadhimisha miaka 30 ya Mapinduzi ya Kiislamu yaliyoongozwa na hayati Imam Khomeini. 357346