IQNA

Mkutano wa uchumi wa Kiislamu na faida zake kwa mustakbali wa Ufaransa kufanyika Paris

8:34 - February 03, 2009
Habari ID: 1739325
Mkutano wa uchumi wa Kiislamu ya faida zake kwa mustakbali wa Ufansa unatazamiwa kufanyika tarehe 12 Februari mjini Paris kwa udhamini wa Jumuiya ya Mawakili na Haki za Kazi (AEMADA) ikishirikiana na skuli ya mawakili wa mahakama za Paris.
Kituo cha Financeislamique kimeripoti kuwa sambamba na kuchunguza nafasi ya uchumi wa Kiislamu kama chombo kipya cha kiuchumi, Wizara za Uchumi, Viwanda na Kazi za Ufaransa, Jumuiya ya Ulaya na Morocco na Mawakili wa Sheria za Kazi wa Ufansa watashiriki pia katika mjadaja wa uchumi wa Kiislamu na faida zake kwa mustakbali wa nchi hiyo.
Lengo la kufanyika mkutano huo limetajwa kuwa ni kuchunguza uchumi wa Kiislamu katika mtazamo wa kishera. 357987

captcha