Gazeti la Daily Times limeripoti kuwa mkutano huo unaosimamiwa na Baraza la Aidiolojia ya Kiislamu la Pakistan unahudhuriwa na mabalozi wa nchi za Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu nchini Pakistan.
Miongoni mwa malengo ya mkutano huo ni kuchunguza masuala muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu hususan katika nchi za Palestina, Afghanistan, Iraq na eneo la Kashmir na kutafuta njia za ufumbuzi wa migogoro ya maeneo hayo. Mkutano huo pia utawasilisha mapendekezo ya utatuzi wa migogoro hiyo kwa jamii ya kimataifa husussan serikali mpya ya Marekani.
Mbali na mabalozi wa nchi mbalimbali, mkutano huo pia unahudhuriwa na wahadhiri mashuhuri na wataalamu wa masuala ya kimataifa.
Matokeo ya mkutano huo yatakusanywa na kukabidhiwa kwa jumuiya husika kote duniani ikiwa ni pamoja ya Umoja wa Ulaya, Jumuiya ya Nchi za Kiislamu na ubalozi wa Marekani mjini Islamabad. 358761